Burudani

Drake awashangaza wanafunzi wa Miami High School

Drake aliamua kutembelea shule ya Miami Senior High iliop[o Florida nchini Marekani mapema jana siku ya Jumatatu kwa ajili ya kushot video ya muziki wake unaoshika nambari 1 ‘God’s Plan’.

Rapa huyo anayetokea Toronto alishot video hiyo sehemu mbalimbali ikiwemo katika ukumbi wa shule na kwenye uwanja wa Baseball. Mmoja wa mashabiki wa Drakew alipost video kwenye mtandao wa Twitter ikionyesha wanafunzi wanavyoimba wakiwa na msisimko.

Ukiachana na swaa la kutengeneza video ya muziki huo, Drake pia aliwasilisha kiasi cha doa 25,000 na aliahidi kuwa atawasaidia kwenye swala la kutengeneza sare zao mpya ya shule. Muda mfupi baada ya kuondoka katika shule hiyo, Drake alionekana kwenye chuo kikuu cha Chuo Kikuu cha Miami na kumzawadia mwanafunzi aitwaye Destiny scholarship yenye thamani ya dola 50,000.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents