Burudani

Drake azuiwa kuingia chumba cha kubadilishia nguo kuwapongeza ‘Miami Heat’ baada ya kujifanya mwandishi wa habari!

Rapper Drake kutoka Toronto, Canada ni mmoja kati ya watu waliofurahia ushindi wa timu ya Miami Heat waliochukua ubingwa wa NBA 2013 Alhamisi (June 20), na katika jitihada zake za kutaka kuwapongeza aliamua kuuweka ustaa kando na kuongozana na waandishi wa habari kuelekea mlango wa chumba cha kubadilishia nguo wachezaji akijifanya naye ni mwandishi lakini walinzi wakampiga STOP!

drake2

Aubrey Drake Graham a.k.a Drake ambaye alikuwa na lengo la kuingia katika chumba cha Miami Heat kwenda kumpa pongezi swahiba wake LeBron James na wachezaji wengine wa Miami, alijikuta akizuiwa na walinzi sababu hakuwa na kibali maalum (media pass).

Kwa mujibu wa Aceshowbiz, mwandishi wa HOOPSWORLD aliyekuwa miongoni mwa waandishi walioongozana na Drake, alitweet akisema kuwa baada ya Drake kuzuiwa na walinzi hao aliwaambia kuwa yeye ni mwandishi wa habari ili wamruhusu!! “Drake was just stopped by security. He tried getting in the locker room without media pass, Drake tried his luck by saying, “I am media.”

Mwandishi mwingine wa Sun-Sentinel naye alitoa maelezo yaliyofanana na hayo “I got in the locker room [and] Drake was denied access,”.

Lakini inavyoonekana hit maker wa ‘Started From The Bottom’ hakukata tamaa ya kuungana na washindi hao wa NBA katika After Party iliyofanyika baadaye usiku huo (June 20) huko South Beach na kuperform hit song yake ‘Started From The Bottom’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents