Burudani

Drake na Chris Brown washtakiwa na klabu ya Wip, watakiwa kulipa dola milioni 16


Wakati ambapo tulidhani kuwa suala hili limeisha, klabu ya usiku ya WiP ya jijini New York Marekani imeibuka na kuwashtaki Drake na Chris Brown kwa kusababisha hasara kubwa mwezi June kufuatia ugomvi wao.
Kwa mujibu wa kesi hiyo, wasanii hao wote waliwasili kwenye klabu hiyo wakiwa na kundi kubwa la watu wakiwemo walinzi, waajiriwa na washkaji na kujumuisha karibu mabaunsa 15 wenye mafunzo maalum ya kupigana.
Hivyo klabu hiyo inataka ilipwe dola milioni 16 kutoka kwa Chris na Drake kwa uzembe, kujihusisha na vitendo vya hatari na kuvunja sheria makusudi.
Katika kesi hiyo iliyopelekwa kwenye mahakama ya Manhattan, klabu hiyo inadai kuwa Chris na Drake “wana uadui uliotokana na kuwa na uhusiano na mwanamke mmoja” uliopelekea wapigane June 14.
Japokuwa maelezo hayo hayajamtaja mwanamke huyo, inaeleweka wazi kuwa ni Rihanna.
Katika hatua nyingine mchezaji wa kikapu Tony Parker naye aliishitaki klabu hiyo kwa kuumizwa jicho wakati wa ugomvi huo na anadai alipwe fidia ya dola milioni 20.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents