Burudani

Drake na Meek Mill wamaliza bifu lao mbele ya maelfu ya mashabiki wao jukwaani (+video)

Baada ya ma-rapper wawili nchini Marekani Meek Mill na Drake mwaka 2015 kuingia kwenye bifu zito la kutupiana maneno makali, hatimaye wawili hao kwa sasa wamemaliza bifu lao.

Meek Mill na Drake

Wawili hao wameuthibitishia umma jana usiku mjini Boston nchini Marekani  kwenye jukwaa la tamasha la Aubrey and the Three Migos, ambapo Drake alipanda  na kutumbuiza na Drake kisha kukumbatiana na kuonesha ishara kuwa wawili hao kwa sasa ni marafiki.

Meek Mill alipanda jukwaani na kuungana na Drake kisha kuanza kutumbuiza wimbo wa Dreams and Nightmares pamoja huku mamia ya watu wakipiga makelele ya furaha.

Drake na Meek Mill waliingia kwenye bifu kali baada ya mrembo Nicki Minaj kuingia kwenye mahusiano na Meek Mill na kuanza kumtumia vijembe Drake jambo ambalo liliamsha hisia kali kwa Drake na kumjibu Meek Mill kwa wimbo wa Back to Back. Tazama video ya wawili hao wakitumbuiza jana jukwaani

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents