Uncategorized

Drake na mkosi wa kuahirisha show Amsterdam, kwa mara ya pili ahairisha show yake tena sababu hazijajulikana

Rapper kutoka nchini Cnada ambaye amehamishia makazi yake Marekani Aubrey Drake Graham  alimaarufu Drake ameamua kuiahirisha show yake tena katika jiji la Amsterdam nchini Uholanzi.

Show hiyo ya Drake huko katika jiji la Amsterdam ambayo ilitarajiwa ifanyike tarehe 23 Aprili imefutwa, kulingana na tovuti ya Ziggo Dome. Kulingana na wamiliki wa barua pepe hiyo walipokelewa taarifa hiyo, ya show kufutwa kwa sababu ya “mabadiliko katika ratiba ya ziara ya mkali huyo”.

Ripoti za AD. Nyingine mbili zinaonyesha Drake amepanga show ya Amsterdam ifanyike Aprili 25 na 26, kulingana na tovuti ya Ziggo. Sababu ya mabadiliko haya haijulikani bado. Drake anatembelea Uholanzi kama sehemu ya safari yake ya The Assassination Vacation Tour.

Ikumbukwe hali hii kwa Drake sio mara ya kwanza rapper huyo wa Canada kufuta show yake huko Amsterdam. Pia alipangwa kufanyika show kupitia tovuti ya Dome ya Ziggo mwezi Machi 2017, lakini haikufanyika kutokana na kuwa mgonjwa. Mashabiki walisubiri kwa muda wa saa kadhaa lakini Drake hakutokea ndio taarifa zikaja kutokea kuwa anaumwa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents