Tupo Nawe

Ushikaji wa Drake na Nicki Minaj ndio basi tena

Wasanii wawili kutoka nchini Marekani mmoja akizaliwa nchini Canada ambaye ni Drake na mwingine kuzaliwa Trinidad and Tobago ambaye ni Nicki Minaj, inasemkana urafiki wao ndio basi tena. Kupitia ukurasa wa theshaderoom umeonyesha wawili hao ambao inadaiwa waliwahi kuwa kwenye mahusiano kuwa kila mmoja amemu Unffolow mwenzake kwenye ukurasa wa Instagram.

Huku wengine wakienda mbali zaidi wakidai maelewano ya Drake na Meek Mil ndio yaliyosababisha wawili hao kuwa na utofauti kati yao, kwani ikumbukwe kuwa Nicki Minaj alitengana na Meek Mil na baada ya kutoka gerezani aliweza kuweka mambo sawa na Drake kwani hawakuwa na maelewano, hiyo ndio ikitajwa kuwa ni sababu kubwa.

Hii ni moja ya screen shoot iliyotolewa kwenye akaunti zao:-

Wawili hao ambao waliingia kwenye game 2009 na kupata mafanikio makubwa wakiwa chini ya lebo ya Young Money ambayo iko chini ya Lil Wayne, toka muda wasanii hawa walionekana kutengana jinsi umaarufu wao ulivyozidi kukua.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW