Michezo

Drogba Kalou Nje ya Ivory Coast

 

Kocha wa Ivory Coast Francois Zahoui hajawajumuisha wachezaji Diddier Drogba na Solomon Kalou katika kikosi chake kitakachochuana na Burundi katika mechi ya awali ya kombe la mataifa ya Afrika 2012 jumamoc wiki hii.

Wachezaji hao wa Chelsea hawakujumuishwa kikosini kutokana na sababu mbali mbali ambazo Zahoui aliziweka wazi.

Kalou hakuitwa kutokana kuwa na majeruhi ya goti huku Drogba akiachwa baada ya yeye mwenye kuomba kutoitwa kikosini.

Inaelezwa kuwa Drogba aliomba asiitwe ili aweze kupata muda wa kurudisha kiwango chake baada ya kua katika majeruhi ya mkono ambayo nusura yamkoseshe kucheza kombe la Dunia mwaka huu.

Badala yake mshambuliaji Kader Keita ameitwa kikosini baada ya kutemwa katika mechi dhidi ya ya Rwanda mjini Abidjan.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents