Michezo

Drogba kulishtaki gazeti la Daily Mail

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Didier Drogba amesema atachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Daily Mail.

7810ccd41bf26faaa2c4e1f20db70a71

Hii ni baada ya gazeti hilo kuchapisha habari zinazodai kwamba kati ya pesa anazokusanya kupitia wasifu wake wa kusaidia jamii, ni chini ya asilimia moja zinazotumiwa kufaa jamii.

Gazeti hilo limesema ni £14,115 pekee kati ya £1.7m zinazotolewa na wachezaji nyota na wafanyabiashara ambazo husaidia watoto Afrika.

Drogba, 38, ametoa taarifa akisema habari hizo ni za “uongo na za kumharibia sifa”.

Tume inayodhibiti mashirika ya kusaidia jamii yaliyosajiliwa Uingereza imesema inachunguza “madai ya ukiukaji wa sheria”.

Kwenye taarifa yake, Drogba amesema: “Hakuna ulaghai, hakuna ufisadi na hakuna udanganyifu.”

Drogba, raia wa Ivory Coast, anayechezea klabu ya Montreal Impact ya Canada kwa sasa amewatuhumu wanahabari wa Daily Mail kwa kuweka hatarini maisha ya maelfu ya watoto wa Afrika.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents