Michezo

Drogba kutundika daluga mwishoni mwa msimu

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba anatarajia kustaafu mchezo wa soka mwishoni mwa msimu wa mwezi Novemba mwaka 2018.

Drogba ambaye kwa sasa anachezea ligi kuu ya Marekani (USL) amesema atastaafu soka mwishoni mwa mwaka 2018 ili kupata muda wa kuendelea na miradi yake mingine ya kimaendeleo.

“Nadhani mwaka ujao utakuwa msimu wangu wa mwisho, nahitaji muda wa kufanya miradi yangu mingine, nafahamu umuhimu wa kucheza lakini kwa umri wangu huu niliyonao wa miaka 39, sioni haja ya kuendelea.” Drogba amekiambia chombo cha habari cha Ufaransa.

Mchezaji huyo wa Ivory Coast amenyakuwa jumla ya mataji manne ya ligi kuu ya Uingereza na tuzo 14 akiwa na Chelsea huku akicheza jumla ya michezo 380 ambapo kwa sasa anaitumikia klabu ya Phoenix Rising ya Marekani.

Drogba kwa sasa amecheza zaidi ya michezo 670 katika timu nane alizowahi kuzitumikia ikiwemo Olympique Marseille na Turkey Galatasaray.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents