Afya

Drogba na Et’oo walivyokasirishwa na madaktari wa Ufaransa kufanya majaribio ya Corona Afrika “Afrika sio yenu mnawaza kuichezea tu” – Video

Drogba na Et'oo walivyokasirishwa na madaktari wa Ufaransa kufanya majaribio ya Corona Afrika "Afrika sio yenu mnawaza kuichezea tu" - Video

Madaktari wawili wa Ufaransa wamevuta hisia za Waafrika na kuonekana kukerwa na kauli zao baada ya kupendekeza kwamba tiba inayowezekana ya matibabu ya Corona inapaswa kupimwa kwanza katika bara la Afrika.

Wakati wa kipindi cha runinga, mmoja wa madaktari hao aliyejulikana kwa jina la Dk. Jean-Paul Mira alisema vipimo hivyo vitatoa matokeo bora endapo utafiti huo utafanywa barani Afrika “hakuna masks” na “hakuna matibabu” wala hakuna mafunzoya kuelekezana”Ikiwa inaweza kuwa kichocheo, haifai sisi kufanya utafiti huu barani Afrika, ambapo hakuna masks, hakuna matibabu, na wala watu hajilindi, kama vile ilivyofanywa katika masomo kadhaa ya UKIMWI, ambapo tulifanya utafiti kupitia makahaba, tunajaribu vitu, kwa sababu wamejaliwa, “Dk Mira alisema.

Mfanyakazi mwenzake, Camille Locht alijibu, akisema kwamba Afrika ambayo haiwezi kupambana na janga hili, inapaswa kutumiwa kama sehemu ya matibabu kwanza kwani “haina nafasi ya kuzuia virusi kwa njia nyingine yoyote”. “Samahani, unakosa hoja hapa. Afrika inahitaji matibabu kwanza, kwani hawana nafasi ya kuzuia Virusi kwa njia nyingine yoyote. Uponyaji hapo kwanza utaokoa zaidi ya watu 100,000 na maisha yao, na hapo kiukweli utaokoa nchi za Ulaya, “Locht alisitishwa.

Baada ya kuonekana kwa matangazo hayo Wakongwe wa soka wa Afrika waliojizolea umaarufu mkubwa duniani kwa umahiri wao wa kucheza soka Didier Drogba kutoka Ivory Coast na Samuel Eto’o kutokea Cameroon wamekuwa wakali baada ya kusikia mpango wa madaktari wa Ufaransa wanaopambana kupata kinga ya virusi vya corona vinayosababisha homa kali ya mapafu.

Eto’o na Drogba wamepinga vikali kuhusiana na maprofesa wawili nchini Ufaransa ambao wamependekeza kuwa majaribio ya kinga ya corona (BCG vaccine) yaje kufanyiwa kwa watu wa Afrika, kitu ambacho kimetafsiriwa na wao kama ubaguzi wa rangi na kuwakosea heshima wa Afrika ambao ni binadamu kama walivyo wazungu.

Eto’o

https://www.instagram.com/p/B-d6SUMCid6/

Staa wa zamani wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Cameroon Samuel Eto’o alionesha hasira zake baada ya kusikia hayo kupitia ukurasa wake wa instagrama kwa kuandika “Nyie ni Wa***, Afrika sio yenu kiasi cha kufikiria mnaweza kuichezea”

Drogba

Kwa upande wa Didier Drogba ambaye amewahi kuichezea Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast kama nahodha aliandika kupitia twitter account yake “Haikubaliki kabisa kuendelea kukubaliana na hili kwa nguvu nakemea hili ubaguzi wa rangi na kuendelea kudharauliwa, tusaidieni kuokoa maisha Afrika na kuzuia kuenea kwa virusi ambavyo vitaenea dunia nzima, badala ya kutuchukulia kama nguruwe”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents