DStv Inogilee!

DStv yaja na ofa ya kuwapandisha wateja wake daraja (+video)

Leo Alhamisi Februari 28, 2019.: Kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia huduma zake za DStv imetangaza tena ofa mpya na kabambe kwa wateja wake inayojulikana kwa jina la “Step Up” ambapo mteja wa DStv atatakiwa kufanya malipo ya mwezi ya kifurushi cha juu ya kile anachotumia na kisha kupatiwa kifurushi cha juu zaidi ya kile alicholipia kwa kipindi cha mwezi mzima bila malipo ya nyongeza.

Akizungumza wakati wa kutangaza ofa hiyo Meneja Uendeshaji wa kampuni ya MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo alieleza kuwa Ofa ya‘Step Up’ ni kampeni maalum kwa wateja wa DStv yenye lengo la kuwatunuku wateja wanaolipia kifurushi cha juu ya kile anachotumia. Wateja wa vifurushi vya Bomba, Family na Compact watakaolipia kifurushi kinachofuatia juu yake watatunukiwa kufurushi cha juu zaidi. Kwa mfano, mteja wa Bomba akilipia kifurushi cha Family atazawadiwa kifurushi cha Compact. Mteja wa Family akilipia Compact anapata kifurushi cha Compact+ na yule wa Compact akilipia Compact+ anapewa kifurushi cha Premium”, alisema Shelukindo.

Aliongeza kuwa “Kampeni hii ya “Step Up” itadumu kwa kipindi cha muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 1 March 2019 hadi tarehe 30 Aprili 2019 na itawahusisha wateja wa Wateja wote ambao akaunti zao hazijakatika vifurushi vya Bomba, Family pamoja na kile cha Compact”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW