Tupo Nawe

DStv yaja na Shangwe za Sikukuu, Watu kununua ving’amuzi vyenye ofa kabambe kwa bei chee (+video)

Kampuni ya MultiChoice Tanzania imetangaza kuzindua rasmi kampeni yake ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama “Shangwe za Sikukuu na DStv” huku ikitangaza ofa kabambe kwa wateja wake wapya wanaojiunga na DStv katika msimu huu.

Mkuu wa Mauzo wa MultiChoice Tanzania Salum Salum amesema ofa hiyo kabambe na ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na watanzania wengi imeanza rasmi tarehe 1 Novemba 2019 hadi 31 Desemba 2019 ambapo wateja wote wapya wa DStv wataunganishwa kwa Sh 99,000 huku wakipatiwa ufundi pamoja na kifurushi cha DStv Compact cha mwezi mmoja bila malipo ya ziada.

Mkuu wa Masoko Baraka Shelukindo amesema kuwa kampuni ya MultiChoice imekuwa na utamaduni wa kushiriki na wananchi katika kunogesha msimu wa sikukuu na kwa mwaka huu wamekuja na kampeni ijulikanayo kama ‘Shangwe za sikukuu na DStv’ ambapo ofa ya mwaka huu inahusisha kifurushi cha Compact cha mwezi mmoja pamoja na kufungiwa bila granama yoyote ya ziada.

“Kila mwisho wa mwaka tunahakikisha tunakuja na kitu kipya ili kuwahakikishia watanzania sikukuu yenye furaha zaidi. Sote tunafahamu wakati huu wa msimu wa sikukuu familia nyingi hujumuika pamoja ambapo shule huwa zimefungwa na watu wengi wakiwa katika mapumziko, huu ndio wakati muafaka wa kuwa na DStv nyumbani ambapo kuna burudani kwa kila mtu” alisema Shelukindo.

Kwa ofa hiyo mteja ana uhakika wa kifurushi cha Compact cha mwezi mzima bila malipo hivyo kuweza kushuhudia burudani kabambe zikiwemo ligikubwa ulimwenguni, katuni motomoto kwa watoto, tamthilia kabambe kama Huba, Kapuni na vipindi vingine mbalimbali bila kusahau chaneli za ndani kama vile TVE, Clouds Plus, Wasafi TV na nyinginezo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW