DStv yawasha moto wa kombe la Dunia 2018!

  • Yatangaza Ofa Kabambe
  • Watangazaji Nguli Kurindima kwa Kiswahili
  • Wateja kutazama popote walipo
  • Mtanange huo kuonyeshwa live kwenye vifurushi vyote
  • Channel maalum 6 kuonyesha Michuano hiyo katika HD

Huku zikiwa zimebaki siku chache kwa kinyang’anyiro cha Kombe la Dunia 2018 kuanza nchini Urusi, Kampuni ya MultiChoice Tanzania (DStv)  imetangaza neema kwa Watanzania kwa kutoa ofa maalum kwa wateja wapya, Sasa wataweza kujiunga na DStv kwa shilingi 79,000 tu na kupata seti ya DStv pamoja na kifurushi cha miezi miwili bure kitakachowawezesha kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia LIVE mechi zote 64  kupitia chaneli sita (6) maalum zilizotengwa kwa ajili ya FIFA Kombe la Dunia 2018 tena katika muonekano angavu yani ni HD.

Na Kwa wale wateja ambao tayari wamekwisha jiunga na DStv, wajiandae kufurahia mashindano ya Kombe la Dunia yatakayorushwa LIVE mechi zote 64 kuanzia kifurushi Bomba kwa sh.19, 000 tu!

Kama hiyo haitoshi, wateja  wa DStv, wataweza kupokea matangazo ya moja kwa moja kwa lugha ya Kiswahiliambapo tuna timu ya watangazaji mahiri wa soka hapa nchini watakaowaletea watanzania burudani hii.

Pia tunapenda kuwakumbusha wateja wetu wote wa DStv kupakua “Download” Application yetu inayofahamika kama “DStv Now “ kwenye simu zao za mkononi ili waweze kufurahia huduma za DStv wakati wowote mahali popote bila malipo ya ziada.

Tunasema “Kama Sio DStv Potezea”!

 

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW