Michezo

DStv yazindua msimu wa mpya wa ‘Soka Mwanzo Mwisho’ (+Video)

DStv yazindua msimu wa mpya wa ‘Soka Mwanzo Mwisho’

Vuguvugu la msimu mpya wa soka linazidi kupamba moto huku maelfu ya washabiki wa soka kote nchini wakisubiri kwa hamu tangazo kutoka DStv ili kujua kuwa je bado wataendelea kupata uhundo wa ligi maarufu duniani kupitia DStv? Swali hilo limepata jibu baada ya MultiChoice kutangaza rasmi kuwa kama ilivyo ada kingamuzi cha DStv kitarusha mubashara mitanange ya ligi maarufu ulimwenguni ikiwemo Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Ligi ya Italia (Serie A ) Ligi ya Hispania (La Liga), ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA Champions League)  pamoja na makombe mengine maarufu duniani.

Pazia la msimu huu mpya wa soka litafunguliwa Jumapili ya Agosti 4 kwa mtanange wa ngao ya Jamii kati ya Liverpool na kigogo wa ligi ya Uingereza Manchester City mchezo ambao utaonyeshwa mubashara kupitia DStv.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Ronald Shelukindo, amesema kuwa msimu huu wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote kuendelea kuliona soka katika muonekano bora zaidi huku wakiweza kufuatilia ligi ya Uingereza yatakayorushwa kwa lugha ya Kiswahili.

Kampeni yetu ya sasa tunasema ni ‘Soka Mwanzo Mwisho’ na tunamaanisha kwani kwa wateja wetu wa DStv, burudani ya soka haitawatindikia kamwe! Ni wapi unaweza kuona mechi zote 380 za ligi ya Uingereza, mechi 380, za ligi kuu ya Hispania, mechi 380 za ligi kuu ya Italia bila kusahau mechi za ligi ya mabingwa Ulaya na nyingine nyingi? Bila shaka ni DStv pekee.. ndiyo sababu tunasema kwetu DStv ni Soka Mwanzo Mwisho!

Katika kuhakikisha kuwa burudani hiyo haimpiti mteja wa DStv, kwa kupitia app ya DStv Now wateja wataweza pia kuangalia popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu, tablet na laptop. Amesema mteja anayetumia DStv Now anaweza kuunganisha vifaa vinne tofauti kwa kutumia akaunti moja bila malipo ya ziada.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wadau wa soka nchini wakiwemo wasanii mbalimbali, wachezaji wastaafu na watangazaji wanaotangaza ligi kuu ya Uingereza kwa Kiswahili ambao ni Salama Jabir, Edo Kumwembe Maulid Kitenge, Ibrahim Masoud (Maestro), Abuubakar Lyongo na Oscar Oscar.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao wa soka wamesema kitendo cha DStv kuonyesha ligi hizo kubwa mubashara ni fursa kubwa siyo kwa washabiki tu wa soka bali pia hata kwa wanasoka wenyewe kwani ni ulingo muhimu wa kujifunza.

Sambamba na uzinduzi wa kampeni hiyo, DStv pia imetangaza ofa maalum kwa wateja wapya wanaojiunga kuanzia tarehe 1 Agosti 2019 hadi 30 Septemba 2019 watajiunga na DStv kwa Tshs. 99,000 / -na kupata kifurushi cha Family cha miezi miwili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents