Bongo Movie

Dude adai ni wasanii wachache wanaonufaika na filamu nchini

Msanii wa filamu nchini, Kulwa Kikumba maarufu kama Dude, amesema tasnia ya filamu inakua ila wasanii wa filamu hawana lolote kutokana na kupata kipato kiduchu kutoka kwa wasambazaji.

1233972_518124004925221_1052866439_n

Akizungumza na Bongo5 leo, Dude amesema wapo waigizaji wachache wananufaika na filamu wanazofanya ila wengi wataendelea kuwa maskini kutokana na mfumo mbaya wa mauzo ya filamu nchini.

“Kuna baadhi ya watu na wadau wa filamu hapa nchini hawataipokea vizuri kauli yangu, especially kwa wasanii wenzangu, nikiwemo mwenyewe nasema sisi hatujitambui kabisa, hivi inawezekana vipi wasanii wote tukatawaliwa na mtu mmoja kama vile mtu aliyeoa wake wengi wasio na maamuzi? Ufanye filamu lazima upeleke kwa wasambazaji wahindi na wanatupeleka wanavyotaka,” amesema Dude.

“Tungekuwa na ushirikiano sisi wasanii tungefika mbali sana, kutokana na filamu jinsi zinavyolipa,lakini kutokana na wasanii wachache wananufaika basi wanajisahau na kuwasahau wenzetu ambao wanalalamika kila siku.Nadhani kama tungeshirikiana wasanii wote tukawa tunauza filamu kwa bei za usawa kutokana na ubora na gharama ya filamu tungefika mbali sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents