Burudani

DUDU BAYA AFUKUZWA KAZI MZUKA RECORD.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Godfrey Tumaini a.k.a Dudu baya (ze Dudu) amejikuta akitemwa katika lebo iliyokuwa ikimshikilia na kumuweka mjini hapa baada ya kile kinachosemekana ni utovu wa nidhamu na kuwa na roho mbaya kwa wasanii na wafanya kazi wenzake kwa ujumla.

Habari za kuaminika kutoka mzuka recodi zimeifikia bongo5

nakusema kua kwa sasa Ze dudu sio msanii anaemilikiwa na lebo hiyo tenab kwani Alisha achishwa kazi na Chonzo chetu cha habari kilisema “dudu siku hizi hayupo tena mzuka record ndio maana hata hii video yake ya sasa haujaona mtu hata mmoja kutoka mzuka record, pia baada ya kufukuzwa kazi alipewa notsi ya kuondoka katika ile nyumba aliyokuwa akiishi kwani ile nyumba inamilikiwa na Art In Tanzania ambyo ni N.G.O. inayomiliki studio ya mzuka record.”

Dudu Baya alikuawa pale mzuka record na Art In Tanzania kama meneja matangazo (promotiona manager) pia alikuwa ni msanii katika studio hiyo ambayo projuza wake ni yule msanii mkongwe wa kundi la mambo jambo anaefahamika kama Benjamini wa mambo jambo. Katika uwepo wake pale mzuka record dudu aliweza kurikodi ngoma kibao tu kama Mimi ni mamba, siwezi kusepa na nyingine kibao tu.

Pia Ze Dudu ametimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi kule maeneo ya tegeta masaiti ambayo alikuwa amepewa nyumba hiyo na mzuka record ili aweze kuishi yeye na familia yake

Katika kusaka hifadhi baada ya kutimuliwa na mzuka record katika nyumba aliyokuwa amepewa aishi yeye na familia yake kule Tegeta maeneo ya masaiti mtu mzima Ze Dudu alijikuta amejikita katika studio ndogo sana na isiyokuwa na jina kabisa hapa mjini , studio hiyo inayomilikiwa na kijana mmoja aneitwa Ras Raja huku studio yake akiita Raja recod ambayo ipo mitaa ya mbezi Africana na kumpa Ze Dudu hifadhi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents