Dudu Baya afunguka mazito kuhusu mwanae, ‘Kawasikilizisha baba zake wengine’

Msanii wa Bongo Flava, Dudu Baya ameonesha kutopendezwa na kitendo cha mwanae, Willy kutoa wimbo bila hata kumsikilizisha.

Dudu Baya amesema Willy angetakiwa kufanya hivyo kwani na yeye ni msanii pia.

“Mimi ni mwanamuziki, yeye ni mwanamuziki na mimi ni baba yake hajawahi kunisikilizisha ngoma ina maana kawasilizisha baba zake wengine,” amesema.

“Kwa hiyo mama yake yeye ndio anajua baba zake wengine ndio maana kawasikilizisha wale, hajaja kuniimbia mimi hata freestyle,” Dudu Baya ameiambia Clouds TV.

Dudu Baya ameongeza kuwa toka ameanza muziki amewasaidia wasanii wengi kupitia project zake mbali mbali kama Dudu Baya Foundation na Dar Scandal na hadi sasa anafanya hivyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW