Burudani

Dudu Baya akerwa na maproducer wanaokopi midundo ya Nigeria

Mamba Dudu Baya amesema mtindo wa baadhi ya watayarishaji wa muziki wa Tanzania wa ‘ku-copy na ku-paste’ midundo ya nje ndio unaharibu muziki wa nyumbani.

Dudu Baya

Rapper huyo ameiambia Bongo5 kuwa watayarishaji anaofikiria kufanya nao kazi kwa sasa ni P.Funk na Manecky.

“Katika watayarishaji wa muziki ambao ninaweza kufanya nao muziki mzuri sasa hivi ni P.Funk na Manecky. Hawa wengine wanaiga muziki wa Nigeria na Afrika Kusini, yaani kazi yao ni copy na paste,” amesema Mamba.

“Mimi ninafsi kazi zangu zitakazokuja kama sio Maneky basi ni P.Funk kwa sababu tukiwaendekeza hawa ndo wanaufelisha muziki wetu. Eti mabadiliko, mabadiliko gani unafanya kwa copy and paste muziki wa mwenzio? Kwanini usifanye chako kwa ubunifu wako? Kwahiyo hawa vijana ndio wanaharibu muziki na kuufanya ufeli. Mbona Ghana wanamuziki wao, Malawi, sisi nini?, Tunatia aibu sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents