Burudani ya Michezo Live

Dudubaya na Kalapina Wazichapa!!

Tokea mwaka huu wa 2006 umeanza hatukubahatika kusikia ugomvi wowote baina ya wasanii wetu kama tulivyozoea,akini katika hali ya kusikitisha na ambayo pia inamhusisha kwa mara nyingine bingwa wa masumbwi miongoni mwa wasanii balaa hilo limeonekana kuanza tena.

Tokea mwaka huu wa 2006 umeanza hatukubahatika kusikia ugomvi wowote baina ya wasanii wetu kama tulivyozoea,akini katika hali ya kusikitisha na ambayo pia inamhusisha kwa mara nyingine bingwa wa masumbwi miongoni mwa wasanii balaa hilo limeonekana kuanza tena.

Mwandishi wetu aliyekuwa akila happy ndani ya ukumbi wa Bilicanas juzi usiku alishuhudia ugomvi mkubwa baina ya wasanii Kalama Masoud, maarufu kama Kalapina na Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ wakichapana makonde ya haja mbele ya umati wa watu waliofika ukumbini hapo kula burudani zao.

Sinema hilo lilianza mnamo saa nane usiku wakati msanii Kalapina kutoka (Kikosi cha Mizinga) alipokuwa akiwapa shavu wasani Nako 2 Nako kutoka A-Town (Arusha) waliokuwa wakiperform usiku huo na ghafla alizuka mpambe mmoja wa Kalapina na kumnong’oneza kitu Kalapina ambapo mara baada ya hapo Kalapina aliweka kipaza sauti pembeni na kumvaa ghafla Dudubaya kwa ngumi mbili za usoni na za kushtukiza kabla ugomvi huo haujaamuliwa na mabouncer wa club hiyo.

Kana kwamba ngumi hizo mbili zilikuwa hazitoshi..Kalapina alisikika akiongea kwa hasira huku akisema…”Ngumi mbili hazimtoshi, niachieni nikamwongeze huyu kazoea, mimi si wa kuchezewa,hawezi kunifanya mimi mjinga kama alivyozoea kuwafanya wengine, nasema niachieni”.

Hata hivyo hadi mwandishi wetu anaondokea eneo la tukio chanzo cha ugomvi huo kilikua hakijajulikana.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW