Burudani

Dully ajitoa

Dully Sykes aka Mr Misifa jana ndani ya crazy friday ya Clouds FM ametamka rasmi kujitoa katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards.

“Nimesema na nilishasema sitaki kuwekwa katika kategory yoyote, sioni faida ya tuzo, sijawahi kupata tuzo tangu nianze mziki, single 36 mpaka sasa kama Salome, Hunifahamu hakuna hata moja nimepata tuzo. Ni bora nitoe single tu na wala hata album sitaki” amesema Dully.

Dully amekuwa msanii wa pili kujitoa baada ya TID kujitoa wiki mbili zilizopita. Kwa sasa Dully yuko katika mazoezi ya band yake ijayo inayoitwa BROTHERMAN BAND MATOOOOOOOUUUUZ.

Habari kutoka kwa DJ Fetty

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents