Dully Atoa Somo

Dully Atoa Somo
Msanii Abdul Sykes ‘Dully Sykes’ ametoa
somo kwa wasanii wachanga kuwa na nidhamu kwa watu wote ili wafikie
mafanikio katika kazi yao ya kimuziki

Ushauri huo ameutoa juzi
alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha mahojiano maalumu na
televisheni moja ya jijini Dar es Salaam.

“Napenda kuwaambia wasanii wachanga wakitaka kufika mbali hawana budi
kuwa na nidhamu katika kazi zao ili wafanikiwe,” alisema.

Dully alisema kwamba sababu ya yeye kuendelea kuwa juu ni nidhamu aliyo nayo kwa watu wote bila kujali ana uwezo gani.

“Nidhamu ndicho hasa kitu kilichoniwezesha kuendelea kuwa juu kila
siku, mara zote kwa watu wanaonijua nimekuwa si kawaida yangu kuacha
kutaniana nao au kuwasalimu,” alisema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents