Burudani

Dully Sykes alia na wasanii waliomtenga kwenye msiba wa baba yake

Wanasema rafiki wa dhati utamjua wakati wa dhiki na tayari Dully Sykes amechuja marafiki wa kweli na feki.

10945261_376250595868934_283166431_n

Dully ambaye wiki hii alimzika baba yake, Mzee Ebby Sykes amesema hatopenda kuendelea kuwatupia lawama wasanii waliomtenga kwenye msiba huo na kwamba hilo anamuachia Mungu.

“Hili suala nilishaambiwa nisizungumze tena kuhusiana na msanii ambaye hajafika, kwahiyo namwachia mwenyezi Mungu,” ameiambia Bongo5.

“Sio tu kwa msanii ambaye hajadhuria wala kuniandikia meseji kwa sababu kuna baadhi ambao hawajafika lakini wako mbali na wameniandikia meseji lakini kuna wasanii ambao niko nao karibu hata meseji hawakuniandikia.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents