Dully Sykes amfunda Alikiba kuhusu maisha ya ndoa

Msanii Dully Sykes amesema Alikiba anapoingia katika maisha ya ndoa anapaswa kuelewa si jambo dogo la kuchukulia kawaida.

Muimbaji huyo ameiambia Planet Bongo, EA Radio kuwa amefurahi sana kusikia Alikiba anaoa binti kutoka Mombasa, Kenya kwani kitendo kicho kinaweza kufanya na yeye akabadili mawazo ya kuoa hapa nchini na kwenda kuoa nje.

“Mimi nampenda Ali mdogo wangu na anajua, namtakia maisha mema kwenye ndoa na namsihi ndoa si kitu kidogo, asikirie ndoa ni kitu kidogo. Anapoamua kumchukua mtoto wa watu hasa ambaye amemtoa nchi nyingine inabidi amheshimu sana, amuonyesha upendo yule mtoto,” amesema Dully Sykes.

Ameongeza kuwa mara baada ya kuona Mr. Blue ameoa amehamasika kufanya hivyo kwani ndoa hiyo imekuwa ikimvutia sana, hivyo na yeye yupo mbioni kufanya hivyo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW