Burudani

Dully Sykes awabeza wasanii wanaofanya kolabo ‘za kimataifa’

Dully Sykes hazitaki mbichi hizi! Muimbaji na mtayarishaji huyo wa muziki amesema hana mpango wa kufanya kolabo na wasanii wa Afrika ambao hawajawahi hata kushiriki kwenye mashindano makubwa ya muziki duniani zikiwemo tuzo za BET.

11385096_893925577317269_399141026_n

Dully ameiambia Story Tatu ya Planet Bongo kupitia East Africa Radio kuwa hatishiki na wasanii wanaofanya kolabo na wasanii wa Afrika ambazo zimekuwa zikiitwa za kimataifa.

“Kwani hao wasanii wa Afrika wamefika international?” alihoji muimbaji huyo.

“Ni wachache ambao wamefika international, maana mtu ambaye anafanya international ni wale waliowahi kushiriki kwenye BET, watu kama Akon vile kafanya wimbo mmoja na Usher Raymond na wasanii tu wakubwa wa Afrika. Hizo ndio kolabo za international.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents