Duma apandishwa Mahakamani kwa kosa la kumtishia uhai msanii wa filamu (Video)

Siku chache baada ya msanii wa filamu @Duma_actor kuonekana kama ameoa, Jumatatu hii amepandishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo Wilaya ya Ilala akituhumiwa kwa makosa mawili chini ya Hakimu, Mhe Rwambali.

Muigizaji huyo amesomewa kosa la kwanza la kumtishia uhai mwigizaji mwenzake wa kike ambaye aliwahi kufanya naye kazi, na kosa la pili ni la madai.

Duma alikana makosa yote mawili huku akieleza kwamba binti huyo anafanya naye kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Hakimu Mhe Rwambali alimuuliza Duma ambaye amekaa maabusu toka Jumamosi kituo Cha Polisi Cha Salender “Huoni ni kosa kumtishia mtu uhai, hata akijikwaa au kupata tatizo lolote utahusika”

Binti huyo aliimbia Mahakama kwamba amekuwa aliogopa hata kutoka nyumbani kwao kutokana na vitisho hivyo.

“Mimi ni mgonjwa, nashindwa hata kwenda hospitali, kuna siku nilitoka nyumbani kwangu watu wakawa wakanifuatilia, na walivyonikuta wakaniambia usipofuta kesi Makamani tutakuonyesha,” alisema binti huyo ambaye jina lake hakutaka liandikwe mtandaoni.

Aliongeza “Kuna ushahidi ambao ninao kwenye simu amesema atanidhalilisha”

Mhe Rwambali ameahirisha kesi hiyo mpaka kesho huku akiwataka wawili hao kila mmoja kuja na vielelezo.

Written and edited by @yasiningitu

 

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW