Habari

Duma atembea muda mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa akitafuta Mke

Dumaa ametembea mwendo mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa nchini India akisafiri urefu wa kilomita 1,300 katika kipindi cha miezi mitano.

Simba marara akitembea

Wataalam wanaamini kwamba mnyama huyo wa kiume anatafuta chakula ama mke.

Duma huyo ambaye amebandikwa mkufu unaoweza kuonyesha kule aliko, aliondoka eneo analoishi katika eneo moja la wanayapori katika jimbo la magharibi la Maharashtra mwezi Juni.

Baadaye alichunguzwa akirudi kupitia mashamba, majini barabarani na kufika katika jimbo jirani.

Kufikia sasa amelumbana na binadamu mara moja baada ya kumjeruhi kimakosa mtu mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa kundi ambalo lilikuwa limeingia msitu ambao mnyama huyo alikua akipumzika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC sswahili, Duma huyo kwa jina C1 alikuwa miongoni mwa watoto watatu waliozaliwa na T1 , Duma jike katika hifadhi ya wanyamapori ya Tipeshwar, ambako ni nyumbani kwa simba marara 10 katika jimbo la Maharashtra.

Aliwekewa mkufu huo wa kielektroniki mnamo mwezi Februari na akaendelea kuzurura msituni hadi wakati wa mvua za upepo mkali ili kutafuta eneo zuri la kuishi.

Ramani inayoonyesha njia iliofuatwa na simba marara huyo
Presentational white space

Mnyama huyo aliondoka katika hifadhi hiyo mwisho wa mwezi Juni, na tangu wakati huo ametembea kupitia wilaya tatu katika jimbo la Maharashtra na jimbo jirani la Telangana.

Wikendi iliopita alionekana katika hifadhi nyengine ya wanyama huko Maharashtra.

Hofu za mawasiliano

Maafisa wa wanyamapori wanasema kwamba hajasafiri kwa mstari mmoja. Anachunguzwa kupitia Setlaiti ya GPS kila saa na amerekodiwa katika zaidi ya maeneo 5000 katika kipindi cha miezi tisa. Duma huyo anatafuta eneo la Chakula na Mke.

Maeneo yanayopendwa sana na mnyama huyo nchini India yamejaa hivyo basi duma wapya wanahitajika kutafuta maeneo mengine, alisema daktari Bilal , mwanabaiolojia mwandamizi wa taasisi ya wanyamapori India aliyozungumza BBC.

Duma huyo hujificha wakati wa mchana na hutembea wakati wa usiku, akiua nguruwe mwitu na ng’ombe kwa lengo la chakula.

Dkt. Habib alithibitisha jeraha moja alilopata mtu aliyeingia katika msitu ambapo duma huyo alikuwa akipumzika, lakini akasema kwamba hakujakuwa na mgogoro wowote dhidi ya bindamu.

Watu hata hawajui kwamba simba marara huyu anatembea karibu na makaazi yao.India inakadiriwa kumiliki zaidi ya silimia 70 ya duma wote duniani

India inakadiriwa kumiliki zaidi ya 70% ya duma wote duniani

‘Hatahivyo maafisa wa wanyama pori wanasema duma huyo atahitaji kukamatwa na kupelekwa karibu na misitu iliopo ili kuzuia ajali zozote

Pia wanahofia watapoteza mawasiliano katika siku za hivi karibuni kwa kuwa betri ya mkufu wa kielektroniki umepungua nguvu kwa asilimia 80.

‘Idadi ya duma imepungua nchini Indi, lakini maeneo wanayoishi pia yamepungua na hakuna chakula’ , wanasema wataalam.

Kila duma anahitaji takriban wanyama 500 katika eneo lake ili kuhakikisha kuna hifadhi ya chakula, wanasema wataalam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents