Michezo

Dunga atangazwa kuwa kocha mpya wa Brazil

Shirikisho la soka la Brazil CBF, limemtangaza aliyekuwa mchezaji wa Brazil, Dunga kuwa kocha wa timu ya taifa kwa mara ya pili.

dunga

Dunga aliyeiongoza Brazil kutwaa kombe la dunia la mwaka wa 1994 aliwahi pia kuwa kocha katika mwaka wa 2006 hadi 2011. Dunga amechukua nafasi ya Luiz Felipe Scolari, ambaye alijiuzulu kufuatia kimbunga cha mabao 7-1 ambayo timu hiyo ililazwa na Ujerumani katika hatua ya nusu fainali .

Scolari mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza Brazil katika semi fainali za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata kichapo kibaya cha mabao masaba kwa moja dhidi ya mabingwa wa kombe la Dunia Ujerumani.

Dunga amewapiku mkufunzi wa kilabu ya Corinthians Tite,Mkufunzi wa kilabu ya Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.

Wachezaji wanamtaka kocha Sabella kuiongoza timu hiyo katika kipute cha kuwania ubingwa wa mataifa ya Amerika ya Kusini yaani 2015 Copa America mashindano yatakayoandaliwa huko Chile

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents