Burudani

Dupy akanusha bifu na The Amaizing

Baada ya kuzagaa tetesi kuwa producer Dupy halipwi fresh na kundi la muziki la The Amaizing linaloundwa na rapa Izo Bizness pamoja na Abela Music, mtayarishaji huyo ameibuka na kueleza kinaga ubaga juu ya stori hizo.

Producer huyo ambaye ametengeneza ngoma kama ‘Tumeoana’ ya kundi hilo, amedai analipwa kila anapofanya kazi na kundi hilo ambapo pia amedai hana tatizo na wasanii wanaounda kundi hilo.

“Hizo ni stori zimetengenezwa, kwanza mie ndio nimetoa jina la The Amaizing, tena nilipigiwa simu na wenyewe wakaniambia kuwa wanaunda kundi linaitwa Amaizing, mie ndio nikasema mbona Amaizing kama linahang nikatoa wekeni The Amaizing, hizo stori zimetengenezwa,” amesema Dupy

Pia producer huyo mwenye maskani yake Mbagala amethibitisha kuwa yeye na Izzo ni good friends na ni kama brother na sio hivyo tu yaani bado wapo pamoja na wanatengeneza mdundo mwingine ambao utakuja kuchukua nafasi ya ‘Tumeoana”.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents