Habari

Eddie Murphy Lives!: Tujifunze kugoogle kabla ya kupost status za maombolezo!


Habari za uongo zimeenea kuwa jamaa amekufa kwenye ajali ya snowboarding (michezo ya kuteleza kwenye barafu) nchini Switzerland.
Wanaziita ‘online death hoaxes’ na Eddie ni latest victim! Ni kitendo cha watu walioshiba ‘ugali’ na kuamua kupika habari za uongo kuwazushia watu maarufu vifo! Jana wabongo kibao wameingia kwenye mtego huu! Mbaya zaidi wengine ni watu maarufu sana ambao tulitegemea wangethibitisha kwanza habari hii kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kabla ya kupost status ndefu kwa mashabiki wao ambao nao huishia kusema tu ‘Rest in Peace blah blah blah!
Mmoja wa watu walioingia mkenge na habari hiyo ya uzushi ni mtangazaji wa Clouds TV Janet Talawa ambaye aliambatanisha picha ya Eddie Murphy na kuandika, “SO!!!!!!!!!…he is also GONE!!!!???????!!!!!!!!!….. mauti yaliyowapata ndugu zangu kwenye ajali ya maji,yaliniumiza sana hata sikujua nitoeje feelings zangu,nikaamua kukaa kimya na maumivu yangu,wenzangu wengi walionyesha machungu yao.
Kweli kabisa!!!kila nafsi na imshukuru Mungu kwakuwa bado hai….hapo ndio napojiona mimi ni makapi tu na hapa napita kama moto wa mshumaa!Namuomba Mungu anisaidie angalau nife kifo chema kwa maana ya anipe angalau nafasi ya kutubu!Mungu awasamehe wenzangu walionitangulia,Naona Wao walikuwa wa maana na muhimu zaidi yangu hapa Duniani. MIMI ni nani hadi leo ananipa Pumzi yake na kuzichulkuwa za wengine wakati bado tunawahitaji?….Kila nafsi itaonja Mauti….kweli neno lake halipiti!ole wetu tusioamini Maandiko.”
Bahati nzuri kuna watu wanaojua mambo haya, wakaamua kumueleza na kumtoa tongotongo machoni, “Hizi habari ni HOAX, mbona zilishasambaa mara nyingi tu. Kwa taarifa yako, Eddie Murphy ni mzima kabisa wa siha njema. Hiyo ajali ni tweeter Hoax ya tokea miaka 4 iliyopita.
Ili surface tena mwanzoni mwa mwezi wa saba (wiki 3) zilizopita. Lakini si taarifa za kweli kabisa (Dativa Shilla).
Ofcourse Dativa yuko sahihi kabisa. Habari hii si ya jana tu! Na pia hiyo si kwanza kuandikwa kuhusu mchekeshaji huyo.
Yafuatayo ni maelezo ya makala ya mtandao wa MTV News yaliyoandika July 12 mwaka huu yenye kichwa cha habari: “Eddie Murphy Lives!: And Other Celebrity Death Hoaxes Debunked.
“Murphy, 51, who has allegedly died a number of times before, including several incidents involving snowboards, is just fine according to reports. He once again fell victim to a rumor spread by the rogue site MediaFetcher, which has been behind bogus stories about the alleged recent deaths of everyone from Jon Bon Jovi to Too $hort, Tiger Woods, Vanilla Ice, Jeff Goldblum, Mac Miller and Charlie Sheen.”
According to E! Online, Murphy is just fine, despite the story spreading like wildfire on Wednesday. Murphy recently walked the carpet with his new girlfriend, “106 & Park” star Rocsi Diaz, at a pre-BET awards party on July 2.
Murphy’s extreme sport death hoax has bubbled up a number of times over the past few months and E! said they can be tied to Internet pranksters at Global Associated News, who have falsely claimed that Goldblum died after falling off a cliff in New Zealand, Adam Sandler bit it during his own snowboarding mishap in Switzerland and Ryan Gosling fell 50 feet to his death from a mountain in the Swiss Alps. (MTV NEWS)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents