Tupo Nawe

Eden Hazard atua Madrid kwa dau la pauni Mil 150, wakala maarufu Mino Raiola yupo huru sasa je atavunja rekodi hiyo ya usajili na nani anafuata ? 

Kila linapofika dirisha la usajili wapo wachezaji ambao wanajiunga na timu mpya na wengine kuondoka jambo ambalo ni kawaida.

Real Madrid have announced the first major signing of the summer in Chelsea's Eden Hazard

Real Madrid imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji waliyekuwa wanamtaka kwa kipindi kirefu Eden Hazard huku macho ya wengi wakiangazia kwa wakala mashuhuri wa wachezaji, Mino Raiola kama ataweza kufanya makubwa baada ya hivi karibuni kutarajiwa kuachiwa huru.

Agent Mino Raiola is expected to see his ban suspended by the Court of Arbitration for Sport

Miamba hiyo ya soka ya Hispania hapo jana usiku siku ya Ijumaa walitangaza kukamilisha usajili wa nyota huyo raia wa Ubelgiji, Hazard baada ya kuitumikia  Chelsea kwa mafanikio makubwa huku akiondoka kwa dau la pauni milioni 150 ambalo halijafikiwa na mchezaji yoyote kwenye dirisha hili la usajili mpaka sasa.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28, ameingia kandarasi ya miaka mitano huku akitarajia kukusanya kitita cha pauni laki nne kwa wiki (400,000).

Raiola ambaye anatumikia adhabu ya FIFA, kwa sasa anashikilia karata moja mkononi ambayo huwenda ikatikisa dirisha hili la usajili. Karata hiyo ni Mfaransa Paul Pogba wakati wengine wanaotarajiwa kushangaza ulimwengu ni pamoja na mchezaji Matthijs De Ligt.

Manchester United midfielder Paul Pogba is one of Raiola's clients and could be affected

Matthijs De Ligt

Matthijs De Ligt ameshaweka wazi maamuzi yake ya kutimkia Amsterdam lakini klabu kubwa Manchester United, Barcelona, Liverpool na Juventus zote zinahusishwa na usajili wa beki huyu mwenyethamani ya la pauni milioni 75.

Paul Pogba

Paul Pogba ameripotiwa kutakiwa kuendelea kusalia ndani ya Manchester United kutokana na pendekezo la kocha, Ole Gunnar Solskjaer lakini Mfaransa huyo mpaka sasa hajaonyesha dalili za kuendelea kusalia.

Real Madrid imekuwa ikihusishwa na kutaka kumsajili nyota huyu hasa kutokana na kocha wao Zinedine Zidane kuweka wazi kutamani kufanya naye kazi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW