Michezo

Edinson Cavani atwaa tuzo hii kubwa mbele ya Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Luis Suarez

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Uruguay, Edinson Cavani ameshinda tuzo ya Golden Foot Award kwa mwaka 2018 iliyofanyika jijini Monaco hapo jana siku ya Jumanne ya Oktoba 30.

Pasipo kutarajiwa na wengi Cavani ameweza kutwaa tuzo hiyo mbele ya wachezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Majina ya wachezaji waliyokuwemo kwenye 10 bora ya kuwania tuzo hiyo ukiachana na Cavani walikuwamo Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich), Lionel Messi (Argentina, Barcelona), Cristiano Ronaldo (Portugal, Juventus), Luis Suarez (Uruguay, Barcelona), Gareth Bale (Wales, Real Madrid), Sergio Ramos (Spain, Real Madrid), Robert Lewandowski (Poland, Bayern Munich), Sergio Aguero (Argentina, Man City) na Thiago Silva (Brazil, PSG).

Related image

Tuzo ya Golden Foot award huwandaliwa na World Champions Club ambapo lengo kuu ni kutambua mafanikio ya wachezaji wa kulipwa ambao wamefanikiwa kucheza kuanzia mechi 28 na kuendelea kuhu mshindi wake hupatikana baada ya kupigiwa kura na umma,vyombo vya habari na watambuzi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents