Burudani

Video: Edu Boy adai video ya wimbo wake ‘Naieee’ iliyoongozwa na Nisher imemgharimu tsh milioni 6

Msanii wa muziki wa Hip Hop Edu Boy amedai video ya wimbo wake mpya ‘Naieee’ iliyoongozwa na director Nisher kutoka Arusha imemgharimu tsh milioni 6.

Muongozaji huyo ndio video yake ya kwanza ndani ya mwaka 2017 baada ya ukimya wa muda mrefu ambao uliwafanya mashabiki kuhisi huwenda ameachana na kazi hiyo.

“Labda niseme video yangu mpaka inakamilika ime-cost kama milioni 6 hivi,” alisema Edu Boy. “Gharama za kumlipa Nisher, pia tulisafiri kule Arusha, hotel, kula na pia baada ya kufika kule tukawa tumechelewa Nisher akakataa kushoot ikabidi tulipie tena location. Kwa hiyo kwa gharama zote mpaka video inakamilika ni milioni 6,”

Rapa huyo ambaye ni zao la Serengeziti Fiesta Super Nyota, amedai video hiyo ndio video yake ya kwanza kumgharimu pesa nyingi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents