Burudani

Edu Boy afafanua wasanii kurekodi bure katika studio yake

Msanii Bongo Flava, Edu Boy amefunguka taarifa za wasanii kurekodi bure katika studio yake ambayo ametangaza kuifungua hivi karibuni.

Rapper huyo kutoka mkoani Mwanza wiki iliyopita alitangaza ujio wa studio yake ambayo itakuwa mkoani humo kwa ajili ya kuwasaidia wasanii wenye uwezo mkubwa wanaochipukia lakini hawana uwezo.

Akizungumza na Bongo5 Edu Boy amesema kuwa si msanii yeyote anaweza kurekodi kwa vile ni bure, bali msanii husika awe na uwezo mkubwa ambao unaweza kushawishi watu kumkubali.

“Tukizungumzia uwezo awe na uwezo kweli wa kuimba, ni msanii yeyote awe wa kuimba au kurap ilimradi anafanya vizuri ,” amesema Edu Boy.

Hata hivyo ameongeza kuwa yeye atasaidia katika upande wa audio pekee kwa ajili ya kutangaza wasanii hao na upande wa video itabidi watafute utaratibu mwingine.

Pia ameeleza kuwa gharama za uwekezaji katika studio hiyo anatengemea zitarejea kupitia matangazo ya kibiashara yatakayokuwa yanafanyika katika studio hiyo, hata hivyo hajaweka wazi ni kiasi gani cha fedha alichowekeza hadi sasa.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents