Burudani

Edu Boy alikitamani kiitikio cha ‘Mazoea’ kwenye ‘Naiee’

Kumbe Edu Boy alikitamani kiitikio cha wimbo wa ‘Mazoea’ wa Bill Nas kukitumia katika wimbo wake wa Naiee! Yes, Habari ndio hiyo!

Akiongea katika kipindi cha Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita, Edu amesema baada ya kurekodi kiitikio cha wimbo huo kwa siku tatu, na producer Mona kukikataa na kumshauri amshirikishe Bill, ndipo alipomfuata rapper huyo na kumshawishi kuhusu jambo la kuhamisha chorus hiyo.

“Nilivyoenda kwa Mona kurecord ile chorus siku ya kwanza Mona kaikataa, nilivyorecord siku ya pili Mona kaikataa, nilirecord siku ya tatu Mona akaikata, nikasema sasa kama unaikataa chorus tutafanyaje? Akasema ukifanya na Bill Nas itakuwa chemistry kali sana,” amesema Edu.

“Tena Bill Nas nilimuomba anifanyie chorus ya ‘Mazoea, nikamfata Bill Nas nikamwambia naomba unifanyie ile chorus ya ‘Mazoea uihamishie humu kwa sababu ile ngoma alikuwa hajaiachia akaniambia hamna Edu Boy, naweza kufanya kikubwa zaidi ya kile endapo utaniamini,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents