Habari

El Chapo alalamika kutopewa nafasi ya kusali gerezani Marekani

Mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya raia wa Mexico, Joaquin Guzman maarufu kwa jina la El Chapo amelalamika mazingira magumu kwenye gereza alilofungwa nchini Marekani.

El Chapo anadai ombi lake la kupewa padre anayezungumzia kihispania limetolewa nje hivyo hana uhuru wa kusali. Wanasheria wa Chapo wameandika barua kwa jaji kuhusu mazingira magumu aliyonayo gerezani, Manhattan’s Metropolitan Correctional Center.

Wanasheria wake wanasema ananyimwa uhuru wake wa kikatiba. Pia wanasema mteja wao ameshikiliwa katika mazingira magumu na yenye vizuizi vikubwa kuliko mfungwa yeyote aliyefungwa Marekani.

Guzman, aliyewahi kutoroka mara mbili kwenye magereza yenye ulinzi mkali Mexico, haruhusiwi hata kushikana mikono na wanasheria wake na hawezi kununua maji ya chupa. ia kwenye chumba alichofungiwa hawezi hata kujua kama ni usiku ama mchana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents