Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

El Chapo awaajiri mawakili maarufu kwa kushinda kesi nzito duniani

Mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya raia wa Mexico, Joaquin Guzman maarufu kwa jina la El Chapo amewaajiri mawakili wengine wawili ambao ni maarufu duniani kwa kushinda kesi nzito.

Mawakili hao waliopewa nafasi hiyo na El Chapo ni Jeffrey Lichtman ambaye alimuokoa John Gotti kutokwenda jela kwa kesi ya mauaji mwaka 2005 pamoja na wakili mwengine Marc Fernich.


Wakili Jeffrey Lichtman aliyeteuliwa kumtetea El Chapo

Akiongea na shirika la habari la NBC baada ya kufanyiwa uteuzi huo, Lichtman amesema, “Hatuingii katika kesi hii kwa matumaini yoyote isipokuwa ukweli kwamba tunatarajia kesi ya haki. Mtazamo wangu daima umekuwa ni kwamba jurusi (watu wanaomsaidia hakimu kwenye kesi mahakamani) huchukua viapo vyao kwa uzito sana na sina shaka tutakuwa na juri ambalo litakuwa na nia ya kuweka akili wazi na kusikiliza ushahidi.”

Guzman, aliyewahi kutoroka mara mbili kwenye magereza yenye ulinzi mkali Mexico, na baadae kuhamishiwa nchini Marekani huku kesi yake inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi April mwakani.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW