Michezo

El clasico kupigwa Marekani leo

Michuano ya International Champions Cup (ICC) inatarajia kuendelea usiku wa kuamkia kesho kwa kuwakutanisha miamba ya soka ya Hispania klabu ya Real Madrid dhidi ya Barcelona.

Madrid na Barcelona zinatarajia kukutana katika kipindi hiki ambacho zipo katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi ya Hispania. Mchezo huo unaojulikana kama  El Clasico unatarajiwa kupigwa mishale ya saa 09:05 Usiku wa kuamkia kesho Jumapili  katika dimba la Hard Rock  lenye uwezo wa kuingiza watu 65,000 lililopo Miami, Florida nchini Marekani.

Katika mchezo huo Madrid itamkosa mchezaji, Cristiano Ronaldo ambaye bado yupo likizo baada ya kutoka katika michuano ya Confederations Cup alipokuwa na timu yake ya taifa ya Ureno.

Gareth Bale ambaye hivi karibuni amehusishwa kuhitajika na Manchester United mwanzoni mwa wiki hii atakiongoza kikosi cha  Zinedine Zindane akiwa sambamba na Karim Benzema pamoja na Isco.

Wakati kikosi cha Barcelona kikiwa kimetimia kwa kuwepo wachezaji, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar .

Naye kiungo wa Barc, Andrés Iniesta amesema kuwa hutakuwa mchezo mzuri kwa wote hasa ukizingatia unachezwa nje ya ardhi ya Hispania.

“Ni kitukigeni kiasi kucheza na Madrid katika michezo ya kujiandaa na ligi tena mbali na nyumbani. Yote ni sehemu ya maandalizi yetu na utakuwa mchezo mzuri na maalumu kwakuwa ni Clasico. Naamini tuta wafurahisha.” Amesema hayo Iniesta.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents