Michezo

Elias Maguli asaini klabu ya KMC inayoshiriki ligi kuu 

Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Elias Maguli amejiunga na klabu ya Manispaa ya Kinondoni KMC, kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya KMC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara zinasema kuwa usajili wa nyota huyo unatokana na pendekezo la kocha wao, Ettiene Ndayiragije ikiwa ni katika jitihada za kuendelea kuimalisha kikosi chao.

Licha ya usajili huo, klabu hiyo imesema bado inaendelea na mazungumzo na nyota kadhaa kutoka klabu mbalimbali na kutarajia kuwatangaza baada ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa ifikapo Novemba 15, mwaka huu.

https://www.instagram.com/p/BqHkLPtDt8_/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents