Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Elizabeth ‘Lulu’ Michael amepata dili nono

Muigizaji kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Elizabeth ‘Lulu ‘ Michael amepata dili la kuwa balozi wa (SZIFF) Sinema Zetu International Festival kwa mwaka 2017/2018

Lulu ambaye aliwahi kupata tuzo ya AMVCA mwaka 2016 katika kipengere cha ‘Best Movie East African’ kupitia filamu yake ‘Mapenzi ya Mungu’, ametoa shukrani zake kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa waandaji wa tuzo hizo zilizoandaliwa na kituo cha Senema Zetu kwa kumpatia nafasi hiyo.

Oct 2/2017…..Azam TV Kupitia Chaneli Ya Sinema Zetu Imezindua Rasmi Tamasha La Tuzo Za Filamu Kwa Upande Wa Africa Mashariki
SINEMA ZETU INTERNATIONAL FILM FESTIVAL (SZIFF)
Hizi ni Tuzo Zitakazo Husisha Waandaaji Na Wadau Wa Filamu Tanzania.
Ni Tuzo Za Filamu Kupitia Televisheni Zenye Nia Ya Kuleta Mapinduzi Katika Soko La Filamu Nchini Tanzania.
.
.
Nitoe Shukrani Za Dhati Kabisa Kwa Uongozi Mzima Wa Azam TV Kwa Heshima Niliyopewa Ya Kuwa Balozi Wa Tuzo Hizi.
Hii Ikimaanisha Kuwakilisha Tasnia Nzima Ya Filamu Katika Tuzo Hizi
.
.
Mwisho Nitoe Wito Kwa Waandaaji Pamoja Na Wadau Wa Filamu Kufatilia Na Kushiriki Katika Tuzo Hizi.
Cc @sinemazetu103
#hakikanizakwetu

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW