Habari

Elton John: Sijiungi na Twitter ng’o!


Sir Elton John anadhani anaweza akaashia jela buree iwapo akijiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter, kisa eti ‘mdomo wake mchafu’ unaweza ukamuingiza kwenye matatizo makubwa.
Mwanamuziki huyo wa Uingereza mwenye miaka 65, anakataa katakata kujiunga na mtandao huo kwakuwa anajua akifanya hivyo atajikuta akizinguana na watu kila kukicha.
Alisema: “Utamaliza career yangu. Nitajikuta jela baada ya siku mbili tu. I mean, no, God almighty. Me and my big mouth, no thank you. That would be the end of the career.”
Hata kama akijiunga na twitter, Elton ambaye ana mtoto mwenye miezi 18 aitwaye Zachary (kwa adoption) na mumewe David Furnish anakubali kuwa atauona mgumu kwakuwa technolojia hiyo mpya imempita kushoto.
Akiongea na gazeti la The Sun, Elton amesema, “huwezi kuniskia nikifanya rekodi ya disco, ya dance ama zingine za aina hiyo kwasababu sijui jinsi ya kufanya. Mimi ni mwoga wa technolojia. Nina iPad lakini sina simu. Si mzuri kwenye computer, kwanza sina.”
“Kila kitu nakiandika chini – nimetoka kwenye wakati tofauti. Nakubaliana na mabadiliko na nafahamu kuwa hiyo ndo future ilivyo, lakini sijui jinsi ya kufanya.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents