Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Eminem atumia dakika 5 kumshambulia Rais Trump kwa matusi (+Video)

Rapa Eminem kutoka marekani ametumia dakika 5 kumshushia maneno makali Rais Donald Trump akihusisha matukio ya Kibaguzi, na hatua zake za ujenzi wa ukuta kutenganisha Marekani na Canada huku akiwapongeza wachezaji wa NFL kwa kuendelea na msimamo wao kupinga vitendo vya kibaguzi kwa kugoma kuimba wimbo wa taifa.

Rais wa Marekani, Donald Trump na Eminem

Eminem kwenye Cypher hiyo amesikika akisema “Ubaguzi wa rangi umekuwa ni jambo zuri kwa Kiongozi wetu (Trump).”

Eminem ameendelea kusema “-Nitaendelea kuponda upuuzi huu unaofanywa wa kujenga ukuta mpaka nitakapoeleweka”

“-Na nitaendelea kuwatukana “F*** You” wote mashabiki na marapa wanaomsapoti rais wa awamu ya 45 (Donald Trump) ”

Hata hivyo, Eminem amemaliza Cypher yake kwa kumshambulia Trump juu ya maamuzi yake ya kutaka kumaliza mzozo wa Marekani na Korea Kaskazini kwa njia ya vita kwa kusema  “-Tunaipenda nchi yetu na tunalipenda jeshi letu, Lakini tunakuchukia sana wewe (….Tusi..) Trump”.

SOMA ZAIDI- Kendrick Lamar, Cardi B na Dj Khaled wang’ara BET Hip Hop Awards 2017

Tazama cypher hiyo ambayo ilikuwa maalumu kwa ajili ya utoaji wa tuzo za Hip Hop za kituo cha runinga cha BET. (BETHipHopAwards2017).

 

 

 

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW