Michezo

Emmanuel Adebayor aeleza kilichomfanya aondolewe katika list ya wachezaji wa Tottenham

Mshambuliaji Emmanuel Adebayor aliyekuwa anaichezea klabu ya Tottenham Hotspurs baada ya kuwa kimya sasa kwa muda mrefu na kutoeleza chochote kilichomfanya aondolewe katika list ya wachezaji wa Tottenham Hotspurs watakaoshiriki mechi za mashindano mbalimbali.

312AD37300000578-3452844-image-a-1_1455800756000
Kuelekea mchezo kati ya Spurs dhidi ya Crystal Palace ambayo anaichezea Adebayor kwa sasa amefunguka hali ilivyokuwa

2CC8B5EB00000578-3452844-image-a-15_1455800932026
Adebayor blames Tottenham Hotspur chairman Daniel Levy

Adebayor alikaa bila timu kwa zaidi ya miezi miwili na kuendelea kulipwa mshahara kama mkataba wake ulivyo kuwa unaeleza, licha ya kuwa hachezi. Katika dirisha dogo la January 2016 Adebayor alijiunga na klabu ya Crystal Palace, February 18 Adebayor kaeleza hali ilivyokuwa na kusema wala tatizo halikuwa kwa kocha wa Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino kama wengi wanavyo dhani bali ni kwa mwenyekiti wa Tottenham Hotspurs Daniel Levy.

“Kiukweli sikuwa na mahusiano mazuri na mwenyekiti wa klabu Daniel Levy, kwani alifanya mambo yawe magumu, lakini mwisho wa siku nilijua mimi ni nani natoka wapi na una panga kwenda wapi, watu wanaweza kukujaji lakini nilijua mimi nataka nini na nimesimama katika msimamo upi, kiukweli nilikuwa na mahusiano mazuri sana na Mauricio Pochettino ila mwisho wa siku ili bidi aniambie kuwa hawezi kunijumuisha katika timu na nilielewa kuwa maisha yangu Spurs yameisha” alisema Adebayor

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents