Michezo

Emmanuel Adebayor aondoka rasmi Tottenham

Mshambuliaji wa kilabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayor 31 hatimaye ameondoka rasmi katika klabu hiyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Adebayo

Mchezaji huyo alikuwa hajaichezea Spurs msimu huu na alikuwa amewachwa katika vikosi vya kucheza ligi ya Uingereza pamoja na ile ya Yuropa.

”Tunamuombea mema katika maisha yake ya baadaye’,ilikuwa ni taarifa ya Tottenham.

Adebayor aliyewasili katika kilabu ya Manchester City kwa kitita cha pauni milioni 5 mwaka 2012,alikuwa amesalia na mwaka moja katika kandarasi yake na alikuwa akitaka kulipwa pauni milioni 5 ili kusitisha kandarasi hiyo mapema.

Hatahivyo kilabu ya Tottenham haijatangaza makubaliano ya usitishwaji wa kandarasi hiyo.

Akizungumza mapema juma hili ,kocha mkuu wa Tottenham Mauricio Pochettino alisema kuwa Adebayor hakuwa katika ‘fikra zake’ ama hata mpango wa mbeleni wa timu ya Tottenham.

Source: BBC SWAHILI

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents