Michezo

Emmanuel Adebayor asajiliwa na Crystal Palace

Klabu ya Crystal Palace ya ligi kuu ya England imemsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Togo Emmanuel Adebayor.

Adebayor amesajiliwa na timu hiyo akiwa mchezaji huru kwa mkataba ambao utamuweka chini ya meneja Alan Pardew mpaka mwisho wa msimu huu wa ligi.

Adebayor

Mshambuliaji huyu mwenye umri wa 31 aliachwa na timu yake ya Tottenham mwezi Septemba mwaka jana, na amefunga jumla ya magoli 94 katika Ligi ya England akiwa amezichezea timu za Tottenham,Arsenal na Manchester City.

Mara ya mwisho kucheza mchezo wa ligi ilikua ni mwezi mei mwaka jana katika mchezo kati ya timu yake ya Tottenham na Man City .

Adebayor ambaye alijiunga na Arsenal, akitokea klabu ya Monaco, ya Ufaransa.baadae akajiunga na Man City kabla ya kupelekwa kwa mkopo kwa miamba wa soka wa Hispania Real Madrid na mwaka 2012 akajiunga na Tottenham.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents