Michezo

Emmanuel Okwi atua Dar kuungana na Yanga

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Uganda, Emmanuel Okwi amewasili leo mchana majira ya saa 9:45 katika uwanja wa ndege wa JK Nyerere akitokea Kampala kwa shirika la ndege la Rwanda Air.

okwi
Okwi akilakiwa na mashabiki wa Yanga baada ya kuwasili Dar

Okwi amekuja kujiunga na klabu ya Yanga SC atakayoanza kuitumikia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa. Mara baada ya kuwasili JNIA Okwi alipokelewa na viongozi wa kamati ya mashindano sambamba na mashabiki, wapenzi na wadau wa soka kwa ujumla.

Akiongea na waandishi wa habari uwanjani hapo, Okwi amesema anashukuru kwa kufika salama jijini Dar es Salaam na hasa katika timu yake mpya ya Yanga. Ameahidi kucheza kwa uwezo wake wote kuhakikisha anaisaidia timu yake mpya kufanya vizuri katika mashindano yote.

Source: Young Africans

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents