Michezo

Emmanuel Okwi yupo fiti – Simba SC

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Okwi anaendelea vema  kiafya baada ya kupata majeraha katika mchezo wa hapo jana Ruvu Shooting  hali iliyompelekea kushindwa kumaliza dakika 90.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba zinasema kuwa mshambuliaji huyo hatari na anayeongoza kwa idadi ya mabao katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara anaendelea vema na angekuwemo katika kikosi kitacho ingia mazoezini jioni ya leo.

Emmanuel Okwi anaendelea vizuri na leo jioni atafanya mazoezi na kikosi cha Simba. Mazoezi yatafanyika katika uwanja wa Boko jijini Dar es Salaam.

Okwi jana alishindwa kumaliza mchezo baada ya kutoka nje kutokana na kupata majeraha kwenye shingo ambayo yalisababishwa mchezo usio wa kiungwana katika mchezo wa soka na mchezaji wa Ruvu Shooting Mau Bodi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents