Eric Omondi aachia parody ya ‘A Boy From Tandale’ ya Diamond

Albamu ya A Boy From Tandale ya Diamond ambayo imetajwa kutoka tangu mwaka jana inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa muziki kutokana na kile kilichosemwa kuwa baadhi ya wasanii wakubwa duniani watasikika ambapo wengine tayari wameshasikika akiwemo Rick Ross na Ne-Yo.

Wakati hilo likiwa linasubiriwa kwa hamu kubwa, mchekeshaji kutoka Kenya Eric Omondi ameona hilo linachelewa na kuamua kuleta parody ya albamu ya nyimbo hizo.

Katika parody hiyo Omondi ameweka nyimbo saba za msanii huyo ikiwemo ‘Nitareje’ aliyomshirikisha Hawa, ‘Mdogo Mdogo’, ‘Mbagala’, ‘Salome’ aliyomshirikisha Rayvanny, ‘Utanipenda’, ‘Sikomi’ na ‘Waka’ aliyomshirikisha Rick Ross.

https://youtu.be/fz34ru19gP8

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW