Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Eric Omondi afunguka alivyoteseka kwenye Uchekeshaji

Mchumia juani hulia kivulini. Eric Omondi kutoka nchini Kenya amefunguka mwanzoni alivyoteseka katika tasnia ya uchekeshaji.

Akiongea na kipindi cha Word Is, Eric amesema kuwa wakati anaanza kufanya kazi ya uchekeshaji alikuwa analipwa kwa kupewa chakula.

“Sekta ya comedy inaenda mahali nzuri. Wakati naanza kufanya komedi, tulikuwa tunalipwakwa chakula. Sasa hivi inalipa. Wazazi wanahitaji kuwatia moyo watoto wao. Komedi inalipa na baadae kuna mwanga mzuri,” amesema Omondi.

“Show yangu mbaya zaidi ilikuwa ni Malindi. Ilikuwa ni mara ya kwanza watu waliokuwa wananiona. Nilikwenda huko na nilichelewa. Nilichukua mic na nilikuwa kama ‘Hawayunii’. Kwa masaa mawili hakuna mtu aliyecheka. Siwezi kusahau siku hiyo,” ameongeza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW