Michezo

Eriksson: Uingereza itashinda ubingwa wa Euro 2016

Meneja wa zamani wa Uingereza, Sven-Goran Eriksson anaamini kuwa timu hiyo inauwezo wa kushinda Euro 2016 msimu huu.
Lakini raia huyo wa Sweden aliyeiongoza Uingereza katika mashindano muhimu mara tatu katika miaka mitano ndani ya timu hiyo amesema kikosi hicho cha Roy Hodgson lazima wajifunze kukabiliana na shinikizo wananolipata wakati wa upigaji mikwaju ya adhabu (penalti) kama watataka kuibuka na ushindi nchini Ufaransa. ”Wana kikosi kizuri,”alisema.Katika hatua ya kufuzu walifanya vizuri,walishinda kilakitu na kwa njia ya kipekee kabisa.wanacheza soka la kuvutia pia,kwanini wasishinde?

150506114710_sven_china_gch_624x351_ap_nocredit

Uingereza walishinda michezo yote kumi katika hatua ya kufuzu michuano hiyo itakayopigwa nchini Ufaransa na kumaliza wakiwa kileleni kwa alama tisa tofauti katika kundi lake.

Meneja Hodson atakitaja kikosi chake chenye wachezaji 23 siku ya jumatatu baada ya kujipa siku nne zaidi kutazama uwezo wa wachezaji wake.

Kama Uingereza watataka kupata ushindi wao wa kwanza tokea mwaka 1966 Eriksson mwenye miaka 68 alisisitiza kuwa ni lazima kushughulikia hali ya upigaji wa penalti. ”Unaongelea upigaji penalti-Uingereza sio maarufu katika hatua hii.wanakua na shinikizo sana katika upigaji. ”Lakini natumai Roy atafanya kazi nzuri na kufikia nusu fainali,fainali ama kuchukua kabisa taji hilo.”

Akiongea na BBC michezo nchini China ambapo kwa sasa anakinoa kikosi cha Shanghai SIPG,Eriksson alisema kuwa Uingereza ilikua timu nzuri katika fainali za kombe la dunia mwaka 2006 na wangepaswa kushinda michuano hiyo iliyofanyika nchini Ujerumani.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents