AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Esma Platnumz ataja sifa za mume anayemwitaji kwa sasa

Dada wa Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameweka wazi sifa za mwanaume ambaye anamwitaji kwa sasa baada ya kuachana na baba watoto wake, Petit Man.

Mrembo huyo ambaye ni mfanyabishara amedai haijati mwanaume wa kujionyesha onyesha mbele ya watu pamoja na kutaka sifa ambazo hazina mpango.

“Mwanaume ambaye namwitaji kwanza awe gentlemen ambaye anaweza akanishauri vitu vingi, labda leo umefungua duka lipo hivi anaweza akawa na wazo lingine, kwahiyo ni mwanaume ambaye atanifanya niende mbali zaidi katika maisha yangu,” Esma aliiambia Wasafi TV.

Aliongeza, “Simpendi mwanaume mwenye sifa ambaye yupo kwaajili ya kujionyesha mbele ya watu na hatekelezi kitu ambacho anakipanga katika maisha yake na kingine sipendi wanaume wa kujionyesha kwa sababu nimeshakuwa nao sana,”

Esma alitangaza kuachana na baba watoto wake huyo bila kutoa sababu. Sio mara ya kwanza wawili hao kuachana na baadaye kurudiana.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW